Kiunjuri amshtumu Raila kuwa anaeneza siasa za propaganda

Waziri wa ugatuzi Mwangi Kiunjuri Photo/File

ad-1

Waziri wa ugatuzi Mwangi Kiunjuri amemshutumu kinara wa ODM Raila Odinga kwa kile anadai anaeneza siasa za propaganda zinazolenga kuwagawa wakenya. Kiunjuri anamtaka Raila kujiuzulu kutoka siasa akisema hana nafasi ya kuliongoza taifa hili. Akizungumza katika kaunti ya Samburu alipotoa chakula cha msaada kwa wananchi, Kiunjuri amemtaka Raila kukoma kuwahadaa wakenya kwamba serikali imeshindwa kukabili ukame ili hali hakutoa suluhu lolote taifa lilipokabiliwa na kiangazia alipokua waziri mkuu.Kwenye hafla hiyo,kiunjuri amedhibitisha wakenya milioni nne wangali wanahitaji msaada wa vyakula kutokana na kiangazi kinachoathiri aeneo tofauti nchini. Hata hivyo amesisitiza serikali imeweka mikakati kuhakikisha hakuna mkenya anaangamia kwa kukosa chakula.amesema shule zote zilizo katika maeneo yanayoathiriwa na kiangazi atapokea gunia 500 za mahindi,gunia 200 za mchele kuhakikisha masomo hayaathiriwi katika shule hizo.

The post Kiunjuri amshtumu Raila kuwa anaeneza siasa za propaganda appeared first on Mediamax Network Limited.


Source: MediaMax Limited

Share this with your FriendsShare on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on Google+0Share on LinkedIn0Email this to someonePrint this page

Post a Comment

You May Also Like

Recommended
Recommended
The government has deployed officials in all maize milling factories…